By Ephantus Mwenda
Add to Cart
Read Preview
"Wakati wa likizo, Mkuki alimsaidia nyanyake kwa kazi mbalimbali kama vile, kuchunga mifugo, kulima shamba lao kubwa na hata kupeleka mazao yao sokoni.
Wanakijiji walimtambua kwa utulivu na bidii yake kikazi na hata shuleni. Mkuki alipenda sana kuwinda katika msitu mkubwa uliokuwa kando ya kijiji chao. Alijua kulenga shabaha ipasavyo na hakuweza kupoteza hata mshale mmoja katika harakati zile. Alipoingia mahali pa kuanzia mawindo yake, paa walijua lazima wangeliwapoteza wenzao wawili au hata zaidi..."
Wakaaji wa kijiji cha Tusonge walioishi kwa umoja, amani na up-endo, walijipata katika janga kuu. Waligundua ya kuwa, watoto wao walikuwa wakipotea wakati wa likizo. Jambo hili liliwatia wasiwasi mwingi kwa sababu kijiji chao kilizungukwa na msitu mkubwa sana na wa kuogofya. Kwa hivyo, walidhania kuwa ni simba ama mash-etani walioishi katika msitu ule waliowala wanao. Hata hivyo, ha-wakufa moyo. Waliamua kutumia mbinu zote wawezazo kung’amua kiini na ukweli wa tatizo hilo.
The Girl From...
Kshs 350.00
Add to Cart
© Matrix Cyber Cafe and Printers 2023.
Developed By Bennito254